Check & Save & Download Instagram user photos and videos. List Most Popular Hashtags and Users. Recent Popular media and share themChecksta
  1. Homepage
  2. @storynzuriiplanet
Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet
Fullname

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Bio 🔵East African Artist 🔥Mr Romantic TANZANIANBOY🇹🇿 Subscribe YouTube channel (storynzuriiplanet) 👇👇👇👇👇

Profile Url

Share
Statistics for "Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet)"
Suggested users for Instagram Profile "Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet)"
HamisaMobetto (@hamisamobetto) Instagram Profile Photohamisamobetto

HamisaMobetto

Irene Uwoya (@ireneuwoya8) Instagram Profile Photoireneuwoya8

Irene Uwoya

Wema Sepetu (@wemasepetu) Instagram Profile Photowemasepetu

Wema Sepetu

👑GEE WORLDWIDE👑 (@gigy_money_og) Instagram Profile Photogigy_money_og

👑GEE WORLDWIDE👑

Chibu  Dangote..! (@diamondplatnumz) Instagram Profile Photodiamondplatnumz

Chibu Dangote..!

millard ayo (@millardayo) Instagram Profile Photomillardayo

millard ayo

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram photos and videos

List of Instagram medias taken by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet)

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA (MWISHO ) SEASON 1  Nilikuwa natembelea vidole. Nilitembezwa kuelekea garini, nilipokaribia gari alinibeba msobems" at Dar es Salaam, Tanzania - 2002241543646591352

SALHA (MWISHO ) SEASON 1 Nilikuwa natembelea vidole. Nilitembezwa kuelekea garini, nilipokaribia gari alinibeba msobemsobe na kuniingiza garini. Nilitaka kupiga kelele, vibao viwili vya nguvu vya kiume vilitua mashavuni mwangu, vibao ambavyo vilinifanya nigugumie kwa maumivu kama nguruwe. Gari lilikata kona kwa nguvu. Safari ya kuelekea kituo cha Polisi ilianza. Tulivyopita usawa wa shule ya msingi Stadium tulipishana na Toyote Prado rangi ya maziwa. Nilipata nafasi ya kuangalia saa yangu, Adam Kimmel origina, ilikuwa ni saa sita na dakika kumi na sita. Nilifumba macho kwa hasira. Machozi yalikuwa yananitoka huku nimefumba macho, nililia kama mtoto mdogo. Kichwani mwangu nilifikiri kwamba ....nilikuwa napishana na milioni hamsini. Nilikuwa natenganishwa na Salha milele. Nilikuwa naongeza idadi ya maadui hapa duniani.... We unafikiri wakina Bizzo wangenielewa kwa kupoteza mzigo wao? Salha kachukuliwa na nani? Mudhakir itakuwaje huko Polisi? Ndani ya Briefcase kuna nini? Kina Bizzo ni kina nani? Kina Vampire wataendelea kuwasaka kina Salha? Na Chunda Mwaseba atakapoingilia itakuwaje? Maswali ni mengine sana lakini season 2 ina majibu.

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 47

Nikiwa sielewi. Nikiwa nimechanganyikiwa. Niifanye ile kazi ama la. Na dau lilikuwa limepanda, milioni thelath" at Dar es Salaam, Tanzania - 2002238369456078206

SALHA 47 Nikiwa sielewi. Nikiwa nimechanganyikiwa. Niifanye ile kazi ama la. Na dau lilikuwa limepanda, milioni thelathini zaidi juu ya zile ishirini alizonambia Bizzo. "Hapa nishaingia choo cha kike. Nilikuwa na uwezo wa kumkatalia Bizzo kabla, lakini sio watu hawa wasioeleweka" Niliwaza kimoyomoyo. Nikajipa moyo "Nayafanya haya yote kwa ajili ya maisha yangu na Salha. Mwanamke ninayempenda kuliko kitu chochote kile. Wacha niende niko tayari kwa lolote, na hii ni kwaajili yako Salha.." Niliinama na kuichukua ile 'brief case' nyeusi. Nilisikia majamaa wote watatu wakipiga makofi ya kunipongeza. Nilitoka nje ya chumba namba nane ndani ya nyumba ya kulala wageni ya Machenza na kuelekea shule ya msingi Stadium, nikiwa na begi langu mkononi, nilipita katika kichochoro kirefu ili kutokea katika njia itakayonipeleka moja kwa moja katika barabara itakayoweza kunifikisha shule ya msingi Stadium. Niliumaliza uchochoro. Nilipofika tu barabarani, mbele ya miguu yangu lilikuwa limesimama gari ndogo ya Polisi huku ikipiga ving'ora kwa fujo. Harakaharaka walishuka askari wanne wakiwa na bunduki mkononi. Zote zilielekezwa kwangu. Nilisimama wima nikiwa na 'brief case' yangu mkononi. Nilichanganyikiwa sana. Ulikuwa wakati wa mashaka kuliko wakati wowote katika maisha yangu. Ulikuwa wakati wa uwoga kuliko wakati wowote katika maisha yangu. Uwoga wa kiwango cha juu. Nilitetemeka haijawahi kutokea hapa duniani. Nilitetemeka vibaya mno. Sikuwa na kosa lolote. Lakini sikujua ni kitu gani kilichokuwemo ndani ya 'brief case' iliyokuwepo mikononi mwangu. Polisi walianza kunisogelea kwa hatua za taratibu. Midomo ya bunduki zao zote zikielekezwa katikati ya kifua changu. Sikuweza kuvumilia, sikuweza katu...Niliyahisi majimaji mepesi ya moto yakitiririka mapajani mwangu, mkojo ulinitoka bila kupenda. Nilijikojolea. Askari mmoja alinizunguka kwa nyuma. Mkono wa kulia akiwa kashika bunduki kubwa, kwa kutumia mkono wa kushoto alinikwida suruali yangu na kuninyanyua juujuu. Nilikuwa natembelea vidole. Nilitembezwa kuelekea garini, nilipokaribia gari alinibeba msobemsobe na kuniingiza garini.

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 46

Picha jinsi nilivyoagana na mpenzi wangu Salha ilinijia kichwani kwangu. Moyo wangu uliingia na ubaridi, ubari" at Dar es Salaam, Tanzania - 2002236598327354920

SALHA 46 Picha jinsi nilivyoagana na mpenzi wangu Salha ilinijia kichwani kwangu. Moyo wangu uliingia na ubaridi, ubaridi wa majuto, ubaridi wa woga. Mara taa ikawashwa! Ndani kukawa na mwanga hafifu ulioletwa na taa ya bluu, taa ya kulalia. Kwa harakaharaka niliwaona watu watatu kwa kutumia ule mwanga hafifu wa bluu. Mmoja alikuwa amekaa juu ya kiti cha mbao, wengine wawili walikuwa wamekaa juu ya kitanda. Cha ajabu, kati ya watu hao sikumuona mtu niliyemtarajia, Bizzo. Woga ulinizidi maradufu. "Karibu kamanda, umekuja on time" Yule jamaa aliyekuwa amekaa katika kiti cha mbao alisema. Sikuitikia. Sikujibu. Nilibaki kimya. Jamaa mmoja aliyekuwa amekaa kitandani alianza kuongea "Umekuja muda mzuri sana mshkaji. Tumepewa sifa zako na Bizzo, na nina uhakika kwa umahiri uliouonesha huko ulikotoka waweza kuifanya kazi yetu kwa ufanisi mkubwa" jamaa aliacha kuongea. Alitoa sigara mfukoni, kisha alichukua kiberiti juu ya meza ndogo iliyokuwepo mle chumbani. Aliwasha ile sigara. Akaivuta funda refu. Aliruhusu moshi mwingi usambae mle chumbani. Akacheka kicheko cha majivuno. "…Saa sita na robo itabidi uwe nje ya geti ya shule ya msingi Stadium. Ukiwa na mzigo ule" Alisema huku akiionesha 'briefcase' nyeusi iliyokuwa imewekwa chini sakafuni. "….saa sita na dakika kumi na sita itasimama gari mbele ya miguu yako. Itakuwa ni Toyota Prado ya rangi ya maziwa. Atatoka mtu upande wa kushoto, sio upande wa dereva, atakuwa amevaa suti nyeusi na miwani ndogo nyeupe, miguuni atakuwa pekupeku, hajavaa viatu. Utamkabidhi mzigo huo hapo uliolala sakafuni. Hatoongea neno lolote. Nawe usiongee neno lolote. Ukishampa ataondoka, nawe utarejea hapa. Nitakukabidhi milioni hamsini baada ya kufanya hiyo kazi kama nilivyokuelekeza",alisema yule jamaa "…sasa hivi ni saa sita kamili" mwengine alidakia "…chukua mzigo peleka, una dakika kumi na tano za kufika shule ya msingi Stadium" mwengine alidakia. Nilibaki nimesimama wima. Nikiwa sielewi. Nikiwa nimechanganyikiwa. Niifanye ile kazi ama la. Na dau lilikuwa limepanda, milioni thelathini zaidi juu ya zile ishirini alizonambia Bizzo.

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 45

Sasa sikia mshkaji wangu, njoo Machenza Guest house saa sita kamili usiku. Usiongeze hata sekunde moja, ni saa" at Dar es Salaam, Tanzania - 2001476113030004825

SALHA 45 Sasa sikia mshkaji wangu, njoo Machenza Guest house saa sita kamili usiku. Usiongeze hata sekunde moja, ni saa sita kamili usiku, ila waweza kuja kabla ya muda huo. Nitakupa mchongo, kesho asubuhi utaamka na zaidi ya shilingi milioni ishirini mkononi, utaenda nje ukiwa na pesa nzuri ya kuanzia maisha" Bizzo alisema kwa kujiamini sana, huku akijikuna pua yake kwa kidole chake cha mwisho cha mkono wa kushoto. Kwa upande wangu, sikuwa na shida ya kwenda South Africa au Malawi. Nilikuwa na shida ya kitu kimoja tu. Pesa. Nilikuwa nahitaji pesa kuliko kitu chochote kile kwa wakati ule. Sikuwa na akiba yoyote ile benki. Mkopo niliouchukua benki kwa kwaajili ya kujengea nyumba yangu uliuteketeza vilivyo mshahara wangu. Sikuwa na njia nyingine ya kupata pesa. Na sasa Bizzo ananiambia habari ya kumiliki shilingi milioni ishirini kwa mkupuo. "Nitakuja Bizzo. Nakuahidi nitakuja. Hebu nielekeze hiyo Machenza Guest House ilipo?" Bizzo alijibu akiwa na furaha sana moyoni mwake."Huwezi kupotea man, ukifika Ilulu stadium muulize msela yoyote yule, atakuelekeza mahali ilipo hiyo guest. Ni guest maarufu sana" Na sasa ndio nilikuwa naelekea chumba namba nane ndani ya guest ya Machenza. Chumba cha Bizzo ili kupewa huo ‘mchongo’ kama ulivyoitwa na Bizzo utakaoniwezesha  kupata shilingi milioni ishirini. Niligonga mlango mara sita. Kama Bizzo alivyonambia garini. "Sukuma tu uko wazi…" Nilisikia sauti kutoka ndani ya chumba namba nane. Nilisukuma mlango kwa woga. Niliuona jinsi mkono wangu mwenyewe ulivyokuwa ukitetemeka. Nikajitosa ndani. Kulikuwa na giza totoro. Sikuweza kumuona mtu yeyote yule, bila kuisikia ile sauti ya awali nisingeamini kama mle kulikuwa na kiumbe chenye uhai. Woga ulinizidi maradufu. Jasho la kwapa lilikuwa linanitoka mfululizo. Mikono yanitetemeka vibaya sana. Nilihisi nimeingia katika hatari. Hatari kubwa sana. Hatari ya kujitakia. Picha jinsi nilivyoagana na mpenzi wangu Salha ilinijia kichwani kwangu. Moyo wangu uliingia na ubaridi, ubaridi wa majuto, ubaridi wa woga. Mara taa ikawashwa!

Check image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 44

Niliangalia saa yangu aina ya Adam Kimmel original. 
Ilikuwa ni saa tano na nusu usiku. 
Nusu saa kabla ya mud" - 2001473176136508895
ReportShareDownload051

SALHA 44 Niliangalia saa yangu aina ya Adam Kimmel original. Ilikuwa ni saa tano na nusu usiku. Nusu saa kabla ya muda wa miadi yetu. Nilimuacha Salha, nikatokomea gizani. Nilisikia kilio cha kwikwi toka kwa Salha. Sikugeuka nyuma. Nilijua nikigeuka nyuma nisingeweza kuondoka. Nilikuwa naenda, naenda kutafuta pesa. Na ilinipasa niende kabla saa sita usiku haijafika. Saa tano na dakika hamsini usiku ilinikuta nikiwa nje ya nyumba ya kulala wageni ya Machenza, kibao cha bluu kilikuwa kinaninginia mlangoni kiliandikwa…Machenza Guest House. Kwa mwendo wa taratibu, kama nilikuwa nalazimishwa na mtu nilienda hadi mapokezi. Nilikutana na dada mmoja akimhudumia mteja. Nilisimama wima nikisubiri zamu yangu ifike. Baada ya kuyaandika maelezo ya yule jamaa kwenye kitabu cha wateja. Alimuelekeza chumba yule mteja, hapo nami nililisogelea dirisha. Baada ya salamu nilimueleza maelezo aliyonipa mwenyeji wangu niyaseme kwake. Na nilimtajia hadi namba ya chumba alichokuwemo mwenyeji wangu. Chumba namba nane. Chumba alichokuwa amepanga kijana niliyekuwa namfahamu kwa jina moja tu, Bizzo. Mhudumu alinielewa, aliniamini, aliniruhusu niende chumba namba nane huku akinionesha mahali kilipo chumba hicho kwa mkono. Bila shaka Bizzo aliacha salamu kwamba atakuwa na mgeni kama alivyoniambia. Nilitembea taratibu sana kuelekea chumba namba nane. Nilitembea huku mawazo lukuki yakikitawala kichwa changu. "Pole sana kwa yote yaliyokukuta Dokta. Na nakwambia hauwezi kuishi kwa raha Bongo kwa hiko kisanga kilichokukuta mshkaji wangu. Cha msingi na cha sekondari hapo ni kusepa nje. Kajichimbie Bondeni huko ama hata Malawi na huyu mtoto mzuri, haya mambo yakipoa utarejea tena Bongo.." Niliikumbuka sauti ya Bizzo ikivyonambia ndani ya gari. Wakati huo Salha akiwa kajilaza magotini kwangu. Nakumbuka nilimuuliza "Sasa mimi nitapata wapi pesa za kuweza kunifikisha South Africa au huko Malawi Bizzo? Yatakiwa niwe na pesa za kutosha ili nisiende kugeuka ombaomba katika nchi za watu" We’ ni mwanaume. Ukifanya mishe utapata mpunga wa kukufikisha huko. Sasa sikia mshkaji wangu, njoo Machenza Guest house saa sita kamili usiku.

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "ALHAMDULLILAH THE UNDERDOG KATIKA UBORA WETU..... @hajismanara @moodewji @simbasctanzania @sokaonline_ @mwanafa @diamond" at Kigamboni Bridge - 2001025559812131753

ALHAMDULLILAH THE UNDERDOG KATIKA UBORA WETU..... @hajismanara @moodewji @simbasctanzania @sokaonline_ @mwanafa @diamondplatnumz

USIRUHUSU WATU KUTUMIA HISTORIA YAKO KUKUNYANYASA! Kuna mambo mengi ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma, kuna hatua nyingi ulipitia, zipo nzuri zipo mbaya, kuna mambo mengi ambayo unatamani kuyasahau katika maisha yako lakini huwezi, kuna mambo mengi unatamani kuyabadilisha katika maisha yako lakini huwezi. Yameshatokea na ni sehemu ya maisha yako, haya tunayaita historia, si sehemu tena ya maisha yako, wewe ni mtu mpya, huwezi kubadilisha historia lakini usijihukumu au kuruhusu watu kukuhukumu kutokana na historia yako. Ulikua Malaya kweli, ulikua mwizi kweli, umetoka katika familia ya kimasikini, ulikua mshamba, ulikua unadanga, ulikua marioo na chochote kile ambacho ulikua, kama umeshapita katika hali yoyote mbaya na sasa hauko huko cha kufanya ni kuangalia historia na kumshukuru Mungu hauko kule tena. Acha kujihukumu, acha kujisikia vibaya na kubwa kabisa usiruhusu watu kukufanya ujisikie vibaya. Anaweza kuwa mume au mke, wanaweza kuwa majirani au ndugu, watataka kukudharau kwakua ulikua flani, watataka kukudhalilisha kwakua unatokea katika hali flani, watataka kukukatisha tamaa kwakua huna elimu flani. Huna haja ya kuwasikiliza, huna sababu ya kuwapa akili yako, wala huna sababu ya kujielezea kwako. Wewe ni mtu mpya hivyo acha kulia, acha kuhuzunika, acha kujiona mbaya, acha kujiona umepungukiwa kwakua tu historia yako si tamu. 🤩

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 43 " Unaenda wapi Muu usiku huu?" Nilimjibu kwa upole "Naenda kutafuta Salha, kutafuta ili tuweze kuishi kesho, tu" at Dar es Salaam, Tanzania - 2000868206219600345

SALHA 43 " Unaenda wapi Muu usiku huu?" Nilimjibu kwa upole "Naenda kutafuta Salha, kutafuta ili tuweze kuishi kesho, tuweze kuishi na kesho kutwa. Lazima tuendelee kuishi Salha ili kutimiza ndoto zetu, na ili tuishi lazima tule mpenzi. Hatuwezi kula bila kuwa na pesa. Naenda kutafuta pesa mpenzi, na.." Salha alinikata kauli "Kutafuta pesa usiku huu Muu?" Salha aliniuliza huku akiinuka. "Wapi utapata pesa usiku huu. Sahivi ni usiku, saa tano usiku. Utaenda kufanya nini ili upate pesa Muu. Tulale, kesho asubuhi tutajua nini cha kufanya" Nilisema tena kwa sauti ya kusisitiza. "Kesho maisha hayaanzi Salha, kesho maisha yataendelea. Lazima tuwe na fedha za kuweza kutuwezesha kuendelea na maisha. Lazima nikasake pesa na nina hakika nitazipata usiku huu. Nakuahidi nitarudi hapa kabla ya saa saba usiku" Niliongea huku nikinyanyuka. Salha nae alinyanyuka. Alinisogelea. Alinikumbatia kwa nguvu. Akanipiga busu katikati ya paji langu la uso. Akanipiga busu tena katika shavu langu la kulia. Akanipiga busu lengine katika shavu langu la kushoto. Akanibusu mdomoni. Midomo yetu iligandana kwa muda. Alitoa ulimi wake. Nikaupokea vizuri kwa ulimi wangu. Nilinyonya ulimi wa Salha. Niliunyonya ulimi mtamu sana kama asali. Tulitumia dakika kumi tukiwa katika hali hiyo. Tukipeana denda. Lilikuwa denda refu zaidi kuwahi kupiga hapa duniani. Tukaachiana. Tuliangaliana usoni. Salha alikuwa analia. Mimi halikadhalika nilikuwa ninalia. "Nakupenda sana Muu", alisema kwa sauti yake nyororo "Nakupenda zaidi Salha" nilimjibu “…nakuahidi nitakupenda siku zote za maisha yangu. Wewe ni shujaa kwangu. Shujaa wangu, shujaa wa kweli. Hakuna mwanaume kama wewe Muu. Wewe ni mwanaume bora sana katika zama hizi. Zama za wanaume wasaliti. Kwangu, wewe ni mwanaume wa pekee sana. Kama kuna mwanamke mwenye bahati basi ni mwanamke anayeishi na wewe Muu, . Na Salha nimeipata hiyo bahati. Sipo tayari kuipoteza hata kitokee nini, alisema Salha." Nilimziba mdomo Salha. Machozi yalikuwa yanambubujika kwa wingi. Nilimuonea huruma sana. Kumuona mwanamke niliyempenda zaidi akilia. Iliniuma sana. Niliangalia saa yangu aina ya Adam Kimmel original. Ilikuwa ni saa tano na nusu usiku.

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 42

Baada ya kutembea kama robo saa kutokea kijiji cha Hoteli tau tuliomba lifti katika lori, lori lililotufikisha" at Dar es Salaam, Tanzania - 2000866406485482182

SALHA 42 Baada ya kutembea kama robo saa kutokea kijiji cha Hoteli tau tuliomba lifti katika lori, lori lililotufikisha katika mji wa Lindi saa mbili usiku. Tulijisikia huru kuwa mbali na wakina Vampire, lakini tulipofikiria maisha yetu yataenda vipi ndani ya Lindi ulitupata woga mkuu. Usiku huo tulipanga kulala katika stendi ya Lindi. Laiti ningejua madhila ya usiku huo haki ya Mungu tusingepanga kulala stendi ya mabasi..au pengine nisingeenda Lindi kabisa. Tulikaa katika kibaraza cha duka moja katika stendi ya mkoa wa Lindi hadi saa tano usiku. Salha alidai amechoka sana. Alikuwa anahitaji kupumzika. Nilitandika maboksi machache mbele ya kile kibaraza cha duka. Nilikaa chini nikiwa nimenyoosha miguu yangu yote miwili. Salha alilala katika miguu yangu. Hazikufika hata dakika sita, Salha alikuwa anakoroma. Sikutaka kukaa mahali pale. Mimi ndiye nilikuwa mwanaume, nilikuwa tegemezi. Ilinipasa kutafuta namna sahihi ya kuona kesho yetu inakuwaje. Nilimuinua Salha taratibu akiwa usingizini, nikamlaza chini ya boksi. Nilimwangalia. Nikainama. Nilikuwa naiangalia sura nzuri sana ya Salha. Ilikuwa imelala kitulivu sana. Sura nzuri, sura nzuri ya mwanamke wa maisha yangu. Nilisogeza mdomo wangu karibu na mdomo wake. Nikambusu. Nilisema kwa sauti ndogo sana "Nakupenda sana Salha. Nakuacha hapa mpenzi lakini nitarudi. Naenda kutafuta baby, nitarudi muda si mrefu” Nilisema kwa sauti kubwa kidogo, karibu na sikio la Salha “…nakuahidi mpenzi, nitakupenda siku zote za maisha yangu. Nitakupenda milele. Nitakupenda kwa kuwa nimeamua kukupenda. Nimekupa moyo wangu Salha. Moyo wangu wote. Nipo tayari kuwa na wewe katika nyakati zote, nyakati za shida kama hizi, nyakati za raha. Amini upo na mtu sahihi, mtu atakayekupigania katika nyakati zote za maisha. Sitothubutu kukuacha peke yako Salha, Sitokutesa hata sekunde moja mpenzi wangu. Siwezi kabisa kumtesa mwanamke ninayempenda sana hapa duni.." Sikumalizia kuongea. Niliona machozi yakitiririka katika mashavu ya Salha. Kumbe alikuwa ananisikia. Alifumbua macho. Tuliangaliana. Alisema kwa sauti ya kwikwi " Unaenda wapi Muu usiku huu?" Nilimjibu kwa upole "Naenda kutafuta Salha,

Check image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 41  Tuliingia katika mashimo, tukianguka na kuinuka. Lakini hatukukoma bado tulizidi kukimbia... Baada ya kukimbia" - 2000166294914592975
ReportShareDownload088

SALHA 41 Tuliingia katika mashimo, tukianguka na kuinuka. Lakini hatukukoma bado tulizidi kukimbia... Baada ya kukimbia kwa muda wa kama nusu saa, tulianza kutembea tena, huku tukiwa makini kusikilizia kama kuna ukelele wa kufuatiliwa kwa nyuma. Kulikuwa kimya. Salha alisema kwa sauti ya kuchoka "Muu nimechoka, nimechoka sana Muu" Nilisema huku ninahema "Najua umechoka mpenzi wangu lakini lazima tukimbie. Kutokukimbia ni kukisubiri kifo. Kifo kibaya sana bila shaka. Lazima tukiepuke kifo kwa kukimbia". Salha alisema kwa sauti ya huruma sana "Daaah sawa Muu lakini..." Nilimshika mkono imara. Haikuwa muda wa majadiliano. Tulitembea gizani harakaharaka. Ulikuwa usiku mbaya sana. Sikuwa nimezoea shurba hata chembe, lakini ilinipasa kujikaza kiume. Tulitembea. Tulitembea. Tulitembea. Tulitembea wee. Tulitembea sana. *************** Lindi Mjini, Alhamis, Desember 17, 2015. Stendi ya Mabasi. Saa 8: 01 P.M MKOA wa Lindi ni miongoni mwa mikoa iliyopo kusini mwa Tanzania. Mikoa mengine ya kusini ni Mtwara na Ruvuma. Ingawa nilizaliwa katika wilaya ya Kilwa na kufanya kazi katika wilaya ya Kilwa, wilaya ambayo ipo ndani ya mkoa wa Lindi, lakini sikuwa nimewahi kufika katika mji wa Lindi, ambao ndio makao makuu ya mkoa wa Lindi. Leo, nilifika Lindi kipindi cha matatizo makuu. Nilifika Lindi kwa shida sana. Nilifika Lindi wakati nilikuwa sina kitu chochote, sina pesa, sina nguo, sina ndugu, lakini nilikuwa na mwanamke aliyenitegemea kwa kila kitu. Sikuwa na hela ya kula lakini nilihitajika kula, pia Salha alikuwa ananitegemea mimi ili ale. Sikuwa na pa’kulala lakini Salha alikuwa ananitegemea mimi juu ya kutafuta sehemu ya kulala. Sikuwa na wakumtegemea, lakini alikuwepo wa kunitegemea, Salha. Tulifika katika mji wa Lindi saa mbili usiku. Baada ya safari ndefu ya kuwakimbia wakina Nassoro. Usiku ule tulipita katika mapori mazito, vichaka vingi sana. Tulitembea maporini zaidi ya saa tano. Tulipatwa na kila aina ya shida. Tulipokuja kuibuka katika kijiji tulijikuta tupo katika kijiji cha Hoteli tatu. Baada ya kutembea kama robo saa kutokea kijiji cha Hoteli tau tuliomba lifti katika lori, lori lililotufikisha katika mji wa Lindi saa mbili usiku.

Check image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 40

Mwanamke aliyepitia mengi sana katika maisha yake. 
Na muungurumo wa gari ulikuwa unazidi. 
Nilihisi Salha aki" - 2000161371959266059
ReportShareDownload075

SALHA 40 Mwanamke aliyepitia mengi sana katika maisha yake. Na muungurumo wa gari ulikuwa unazidi. Nilihisi Salha akitikisika. Mara alianza kuongea peke yake. "Wanakuja, wanakuja, nakwambia wanakuja Muu…" Salha alikuwa anaweweseka. Na pengine ilikuwa kweli wanakuja. Maana sasa nilisikia muungurumo wa magari matatu tofauti. Nilimuamsha Salha taratibu. Alikurupuka kutoka usingizini. Wanakuja Muuuuuuuuu!" Alisema kwa sauti kubwa akiwa amesimama wima. "Tulia Salha. Tuko sehemu hatari, usipige kelele" Nilimwambia kwa sauti ndogo. "Nassoro ni Rick Ross" Salha alipayuka bila kujielewa. Nilinyanyuka harakaharaka. Nikamfata Salha na kumziba mdomo kwa mkono wangu wa kulia, nilihisi Salha bado alikuwa usingizini. Anaweweseka. Macho yalimtoka pima. "Muu, Muu, Muu" Salha alikuwa anajitahidi kuita. Lakini sauti yake haikuweza kutoka kama akivyotaka. Ilipotelea mkononi mwangu. "Tulia Salha, usipige kelele, unajua tupo katikati ya hatari" Nilimwambia kwa kumnong'oneza sikioni. Sasa alinielewa. Alitulia tuli. Sasa nilisikia muungurumo wa pikipiki. "Watakuwa wapo wengi sana" Nilijisemea mwenyewe kimoyomoyo. "Tutoke hapa Muu, sio sehemu salama" Salha alirudi katika akili zake za kawaida. "Yeah ni kweli, lazima tutafute namna ya kutoka hapa. Itakuwa tumezungukwa na maadui wengi sana" Nilimwambia. "Nim..eota Nass…oro an..akuch..inja Mu..u…" Salha alisema kwa sauti ya kutetemeka. "Ndomana ikaitwa ndoto. Haiwezi kuwa kamwe. Nitahakikisha Nassoro anafungwa!" Nilisema kwa kujiamini. "Safi my gentlemen " Salha alisema huku akinipigapiga mgongoni. Mara, tulisikia ukelele wa kukanyagwa majani makavu ya mikorosho karibu kabisa na pale tulipokuwa. Bila shaka kuna mtu au watu walikuwa wanapiga hatua kuja pale tulipokuwa. "Tukimbie Muu" Salha alisema kwa sauti iliyojaa wasiwasi. Nilimshika mkono Salha na kuanza kuelekea mbele. Tulianza kutembea kidogokidogo, mwishowe tukaanza kukimbia. Tulikimbia zaidi ya dakika kumi na tano. Ulikuwa usiku wa shida sana. Tulijigonga na miti mara kadhaa, tulikwaruzwa na miiba. Tuliingia katika mashimo, tukianguka na kuinuka. Lakini hatukukoma bado tulizidi kukimbia...

Check image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 39  Alikuwa anahema vibaya sana. Huku akilia kwa sauti ndogondogo, kilio cha kike, kilio cha kuchoka. Niligeuka ny" - 1999285018435141169
ReportShareDownload187

SALHA 39 Alikuwa anahema vibaya sana. Huku akilia kwa sauti ndogondogo, kilio cha kike, kilio cha kuchoka. Niligeuka nyuma, taa za ile gari hazikuwepo. Tulikata upande wa kulia kuelekea upande ilipo shule ya Sekondari Kilwa. Tulikimbia kidogo, kabla hatujafika mahali ulipokuwepo uwanja wa mpira wa miguu wa shule hiyo, tulikata kushoto. Tukawa tunapita katika shamba kubwa la mikorosho la shule hiyo, tulikuwa tunaipita mikorosho iliyoshonana vyema. Ulikuwa usiku wa manane, usiku wa giza totoro, lakini sikuwa na hofu hata chembe moyoni mwangu. Nilijua pale ndio mahali salama pengine kuliko popote pale kwa wakati huo. Giza ndilo tukilolihitaji zaidi, kutuficha na mkono mbaya wa Vampire pamoja na wakina Nassoro. Tuliendelea kutembea kwa mwendo mdogo wa tahadhari porini. Tulizidi kuelekea mbele. Hali ya pori ilikuwa kimya. Michakato ya miguu yetu tu ndio iliyokuwa inasikika. Hakuna aliyekuwa anaongea, ilikuwa inasikika mihemo na pumzi zetu tu. Niliangalia saa yangu ya mkononi, saa aina ya Adam Kimmel original, ilikuwaa ni saa saba na dakika sita usiku. "Nimechoka sana Muu, naomba tupumzike" Salha alisema kwa sauti ya kuchoka kweli. Alikuwa hatanii. Nilimuelewa. Tukapumzika, tulikaa chini ya mti wa mkorosho. Nilinyoosha miguu yangu huku nikiwa nimeliegemea shina la mkorosho. Salha alijilaza katikati ya mapaja yangu. Alidumu macho dakika zisizozidi kumi. Kisha alipitiwa na usingizi. Nilikaa nikiwa nimeegemea shina la mkorosho. Kwangu usingizi haukuja hata kidogo. Nilibaki macho nikitafakari mambo magumu niliyoyapitia siku ile. Taswira ya maiti ya Dokta Martin ilinijia kichwani mwangu. Taswira ya maiti ya nesi Muna aliyeuwawa kinyama ilinijia kichwani mwangu. Nikiwa katikati ya mawazo ghafla nilisikia muungurumo wa gari. Nilitulia tuli. Nikimwangalia Salha usoni. Alikuwa ametopea katika lindi la usingizi. Sura nzuri ya Salha ilikuwa inaonekana vizuri. Weupe wake wa asili uling'ara gizani. Nilimwangalia mwanamke yule mzuri. Mwanamke mwenye urembo usio na mfano. Mwanamke aliyeyashuhudia mengi katika umri wake mdogo. Mwanamke aliyepitia mengi sana katika maisha yake. Na muungurumo wa gari ulikuwa unazidi. Nilihisi Salha akitikisika.

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 38 "Usihofu Salha tutatoka salama" "Tutakimbiaje sasa?" Salha alinielewa, nae aliongea kwa sauti ambayo nilikuwa n" at Dar es Salaam, Tanzania - 1998494503095637121

SALHA 38 "Usihofu Salha tutatoka salama" "Tutakimbiaje sasa?" Salha alinielewa, nae aliongea kwa sauti ambayo nilikuwa naisikia mimi pekee, kisha aliongea kwa sauti kubwa kuijibu ile sauti yangu kubwa.."Sawa Muu. Siogopi" Nikajua Salha ameuelewa mchezo. Sasa tulikuwa tunamchezea shere Vampire kwa maneno popote pale alipokuwa. Tuliongea kwa sauti ndogondogo kwa manufaa yetu, kisha tuliongea kwa sauti kubwa kwa manufaa ya Vampire na washirika wake. Nahesabu hadi tatu kisha tunakimbia kupitia mlangoni" Niliongea kwa sauti ndogo. Kisha nikasema kwa sauti kubwa nilisema "Tukague chumba kimojakimoja. Tumtafute huyo Vampire!" "Sawa Muu" Salha aliitikia kwa pamoja. "Nahesabu hadi tatu kisha tuende" Nilirudia kusema kwa sauti kubwa. "Moja" Nilianza kuhesabu. "Mbili" Tuliacha kukumbatiana. "Tatuuu" Nilisema kwa nguvu. Tulitoka nje ya ukumbi wa Nesi Muna mkukumkuku. Tulifika nje ya mlango na kuanza kukimbia bila uelekeo maalum. Zilikuwa mbio, mbio kweli. Mbio kama za marathon vile. Ijapokuwa ulikuwa usiku wa manane lakini bado umahiri wangu katika mbio ulionekana. Na Salha pia hakuwa lelemama. Tuligeuka nyuma mara kwa mara, lakini hatukumuona mtu. Labda huyo Vampire huko alipo alikuwa anasubiri ukaguzi wetu wa chumba hadi chumba. Sikujua hata tulipita njia gani kutokana na kuchanganyikiwa, lakini akili yangu ilipokaa sawa tulijikuta tupo karibu na shule ya msingi Mnazimmoja. Tuliongeza kasi ya kukimbia kuelekea upande iliopo shule ya Sekondari Kilwa. Tulipofika njia panda kabla hatujafika Dodoli, niliona mwanga wa gari ikitokea upande wa kanisa kubwa la Roman Catholic. Tuliongeza kasi ya kukimbia. Kichwani mwangu lilinijia wazo moja tu. "Range Rover Vogue nyeusi ilikuwa inatufuata" Kila nilivyokuwa ninawaza kwamba gari lililopo nyuma yetu ni Range Rover Vogue nyeusi, basi na kasi ya kukimbia iliongezeka maradufu. Tulivyokaribia mtaa wa Dodoli. Niliushika imara mkono wa Salha. Salha alikuwa anaelekea kuchoka. Niliuona uzito wa mwili wake jinsi nilivyokuwa namvuta. Alikuwa anahema vibaya sana. Huku akilia kwa sauti ndogondogo, kilio cha kike, kilio cha kuchoka. Niligeuka nyuma, taa za ile gari hazikuwepo.

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 37

Ama hakika yule ni mwanamke wa ajabu sana" Nilikuwa naongea kwa sauti ya taratibu, lakini nilikuwa na uhakika " at Dar es Salaam, Tanzania - 1998493586967307234

SALHA 37 Ama hakika yule ni mwanamke wa ajabu sana" Nilikuwa naongea kwa sauti ya taratibu, lakini nilikuwa na uhakika Salha alikuwa ananisikia. "Sio mahali salama hapa Muu. Tuondoke, wanaweza kuja anytime kutumaliza" Salha alishauri. "Kwanini sasa wamuue nesi Muna?" Niliuliza katika hali ya kuchanganyikiwa. "Hutumia akili wale. Itakuwa wana sababu zao za kufanya hivi. Nakuonea huruma sana Muu kwa kukuingiza katika mkasa huu" Salha alisema kwa majuto. "Huna haja ya kunionea huruma. Nafurahi kuingizwa katika hatari na mwanamke ninayempenda zaidi duniani. Naamini tutatoka salama Laaziz" Nilisema kiujasiri na kwa kujiamini sana. Salha alinikumbatia kwa nguvu. Alininong'oneza sikioni huku akiwa kanikumbatia "Nakupenda sana mwanaume wewe…" "Na Vampire anawapenda pia…" Nilistuka sana! Tulisikia sauti kutoka kusikojulikana. Ilikuwa sauti ileile, iliyokuwa inaongea na mimi mchana. Sauti ya mwanamke mrembo sana, lakini katili sana. Mwanamke ambaye sikuwa tayari kabisa kwa sasa kuisikia sauti yake. "Na Vampire anawapenda pia" Maneno ya Vampire yalijirudia tena katika kichwa changu. Tuliachana harakaharaka, toka katika kumbato. Kila mmoja aliangaza huku na huko kutafuta mahali ilipotokea ile sauti. Hatukuona. Na wala hatukuisikia tena. Nilimwangalia Salha, alikuwa anatetemeka pasi na kifani. Alikuwa anaogopa sana. Sauti ya mwanamke anayekwenda kwa jina la Vampire ilimtetemesha sana Salha. Ilimuogopesha sana. "Usiogope Salha, tutatoka salama" Niliongea kwa sauti ndogondogo. Salha alinisogelea. Alinikumbatia kwa nguvu. Niliyasikia mapigo yake ya moyo yakivyopiga kwa nguvu, tena harakaharaka. "Namuogopa sana Vampire, Muu". Alisema tena, kwa sauti ya hofu. Huku akilengwa na machozi. "Usihofu Salha, hapa yatupasa kukimbia. Sio sehemu salama tena" Nilimwambia kwa sauti ndogo sana, sauti ambayo nilikuwa na uhakika alikuwa anaisikia Salha pekee yake, hata Vampire ama mtu yeyote aliyekuwepo mle ndani nilikuwa na uhakika hawezi kuisikia. Kisha niliongea kwa sauti kubwa kidogo ambayo nilikuwa na uhakika Vampire na washirika wake kama walikuwepo walikuwa wanaisikia.."Usihofu Salha tutatoka salama" "Tutakimbiaje sasa?"

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 36  Salha nae alinifata kwa nyuma akiwa kimya. Nilivyofika sebuleni, nilipatwa na mstuko mkubwa sana! 
Sebuleni ku" at Dar es Salaam - 1997936852636961078

SALHA 36 Salha nae alinifata kwa nyuma akiwa kimya. Nilivyofika sebuleni, nilipatwa na mstuko mkubwa sana! Sebuleni kulikuwa na mwili wa mtu umelala chali ndani ya dimbwi la damu!. Mwili ukiwa mtupu kama ulivyozaliwa. Sehemu ya tumbo ya mwili huo kulikuwa na jeraha kubwa na baya sana, kulikuwa na uwazi mpana katika sehemu ya tumbo, bila shaka yule mtu alikuwa ametobolewa tumbo na kutolewa utumbo!. Hakuwa na maziwa kifuani. Maziwa yake yote mawili yalikuwa yamekatwa na kusweka ndani ya lile shimo lililopo pale tumboni. Hakuwa na macho. Alikuwa ametobolewa macho, na damu kutapakaa uso mzima wa yule dada. Kwa chini alikuwa na mguu mmoja, mguu wa kulia, huku mguu wake wa kushoto ukiwa umening'inizwa kwa kamba kutokea darini. Sebuleni palikuwa pananuka damu! Ilihitaji roho katili sana kuweza kuendelea kuiangalia ile maiti mara mbilimbili, kuendelea kuvuta hewa ya mle ndani. Bila shaka yule mwanamke alikuwa amepitia mateso makali sana kabla ya kifo chake... "Ni nani huyo Muu?" Sauti ya iliyojaa woga ya Salha ilinitoa mawazoni. "Ni nesi Muna" Nilijibu kwa sauti ndogo sana. Sauti ya kukata tamaa. Niliuona mstuko wa wazi toka usoni kwa Salha. "Itakuwa Vampire ameshapita hapa!" Salha alisema. Kusikia neno Vampire ule mstuko aliokuwa nao Salha ghafla ulihamia kwangu. Niliikumbuka taswira ya mwanamke yule mrembo sana jinsi nilimvyomkuta katika ofisi ya Dokta Martin akiwa hana wasiwasi wowote, kashamtoa roho zamani. Pamoja na kuwa na uhakika Vampire alikuwa ni muuaji hatari, lakini sikuwaza kama anaweza kuua kikatili namna ile. "We umejuaji kama mauaji haya kayafanya Vampire?" Salha alinyoosha mkono wake kuelekea ukutani. Nami niliyaelekeza huko macho yangu. Niliona mchoro uliochorwa kwa alama nyekundu. Mchoro wa damu. Bila shaka damu ya nesi Muna ilitumika kuchora pale ukutani. Mchoro ule ulikuwa ni herufi kubwa ‘V’. Fikra zangu zilirudi nyuma harakaharaka. Nilikumbuka kuiona alama kama ile katika ofisi ya Dokta Martin. "Yaani Vampire anaua na kuweka chata ya ‘V’ ukutani? Ama hakika yule ni mwanamke wa ajabu sana" Nilikuwa naongea kwa sauti ya taratibu, lakini nilikuwa na uhakika Salha alikuwa ananisikia. "Sio mahali salama hapa Muu.

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 35 "Sasa tutajificha wapi kwa muda huu wa kusubiri huu upepo mbaya upite?" Salha aliniuliza. "Kuna rafiki yangu mm" at Dar es Salaam - 1997930903796904618

SALHA 35 "Sasa tutajificha wapi kwa muda huu wa kusubiri huu upepo mbaya upite?" Salha aliniuliza. "Kuna rafiki yangu mmoja. Ni nesi katika hospitali yetu pale, anaweza kutuhifadhi nyumbani kwake kwa muda" Nilimwambia. "Unamuamini huyo rafiki yako?. Tuko katika wakati mbaya sana, lazima uwe na imani kuu kwa kila mtu utakayemshirikisha katika jambo hili" Salha alinionya. Nesi Muna alikuwa ni zaidi ya rafiki kwangu. Tulikuwa tunashirikiana katika mambo mengi sana. Alinipa siri zake, nilimpa siri zangu. Tulishauriana katika mambo mbalimbali, tulipeana moyo katika matatizo mbalimbali. "Namwamini sana nesi Muna. Ni rafiki yangu mkubwa sana" Nilijibu kwa kujiamini. "Sasa yatupasa kutoka usiku wa manane kuelekea huko nyumbani kwa nesi Muna " Salha alishauri. "Ila si itabidi nimtaarifu kwa simu kama tutaenda nyumbani kwake usiku?" Nilimuuliza Salha. "Hapana, usitumie simu. Wanaweza kuyanasa mazungumzo yenu.Wakatuvizia na kutukamata. Tutam'surprize' tu"Alinijibu."Haiwezi kuwa mbaya hiyo?" Nilimuuliza tena Salha. "Ni nzuri zaidi kwa wakati huu mgumu tuliokuwa nao" Ilipotimu saa sita ya usiku, tulitoka katika kipori kidogo ndani ya pwani ya Jimbiza. Kwa mwendo wa tahadhari kubwa sana tulikuwa tunaelekea nyumbani kwa nesi Muna. Tulikuwa tumeongea mengi sana na Salha. Kuhusu huu mkasa, kuhusu mustakabali wa maisha yetu yatakavyokuwa baada ya kuisha mkasa wa hatari uliotukumba. Nilimuelewa, alinielewa. tulielewana. Saa sita na dakika arobaini na tatu ilitukuta tukiwa nje ya mlango wa nesi Muna. Niligonga mlango taratibu sana, lakini hakuna mtu aliyekuja kutufungulia, niligonga tena, safari hii kwa nguvu kidogo, tofauti na hapo awali, bado ilikuwa kimya, nikagonga tena, safari hii huku nikiita jina la nesi.Muna kwa sauti ndogo.Bado ilikuwa kimya.Ilitokea kama bahati mbaya nikalizungusha komeo la mlango. Mara, mlango ulifunguka! Moyo ulinipiga vibaya sana! "Inamaana Nesi Muna amesahau kufunga mlango leo?Niliwaza kimoyomoyo.Nilianza kuingia ndani huku nikiita kwa sauti ndogo. Salha nae alinifata kwa nyuma akiwa kimya.Nilivyofika sebuleni, nilipatwa na mstuko mkubwa sana! Sebuleni kulikuwa na mwili wa mtu umelala chali ndani ya dimbwi la damu!

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 34

Namba ngeni" Alisema kwa sauti ndogo. "Pokea" Nilimwambia. 
Aliniangalia usoni huku akitikisa kichwa kukataa. " at Uswaz Kwetu - 1997368542757230830
Uswaz Kwetu ReportShareDownload275

SALHA 34 Namba ngeni" Alisema kwa sauti ndogo. "Pokea" Nilimwambia. Aliniangalia usoni huku akitikisa kichwa kukataa. Simu iliita mpaka ikakata. Baada ya dakika mbili simu yake iliita tena. Namba ileile. "Pokea Salha" Nilimshauri tena. "Hapana Muu, ni hatari kupokea simu kwa wakati hatari kama huu" Salha aliongea kwa sauti ndogo. Nilikuwa sijamuelewa Salha. Lakini niliamua kusikiliza hisia zake. Nilitulia tuli nikimwangalia Salha akivyoiangalia simu yake. Simu ilivyokata. Salha aliifungua nyuma ya simu yake. Aliitoa 'line' yake ya simu na kuivunjavunja. "Ni very easy waka'detect tulipo kwa kutumia hizi simu" Salha alisema huku akiiweka mfukoni simu yake isiyo na 'line'. Nilikubali kwa kichwa. Nilikumbuka jinsi ya filamu kadhaa za kimarekani wakivyotumia njia hizo. Lakini sikuwa naamini kama hiyo teknolojia itakuwa imefika hadi Tanzania. Dakika tatu baadae simu yangu ilianza kuita. Ilikuwa namba ileile. Namba iliyotoka kumpigia Salha hivi punde. Nilichukua simu na kumuonesha Salha. Alicheka. "Si unaona, nilikwambia, huyo ni Vampire!" Alisema kwa hamasa. "Kaipataje sasa namba yangu?" Nilimuuliza Salha swali la kizembe. "Nimekwambia huyo ni Vampire!" Salha alisema kwa nguvu. Aliendelea "Yaani usishangae Vampire kujua namba yako, ni kitu kidogo sana kwake" Nilikubali kwa kutikisa kichwa kama zezeta. Mara ya tatu sasa simu yangu ilikuwa inaita. Ilivyokata. Nikaizima. Nikaitia mfukoni. "Sasa tutatokaje hapa. Yatupasa kuwa nje ya mji huu. Mji ushachafuka huu, bila shaka kutakuwa na maadui wengi sana" "Ni kweli yatupasa tuondoke lakini sio sasa. Bila shaka wakina Vampire watahisi sisi tunataka kutoroka. Bila shaka wataweka watu katika njia zote zitakazotuwezesha kutoka katika mji huu. Hapa la msingi tutafute sehemu tutakayoweka kambi yetu ya muda mfupi. Mambo yakitulia ndipo tutaondoka" Salha alinieleza. Nilikubaliana na mawazo ya Salha. Ni kweli ilitupasa kujificha sehemu kwa muda. Ni sehemu gani salama? Ndipo nilipomkumbuka nesi Muna. "Nesi Muna anaweza kutuficha nyumbani kwake kwa muda" Niliwaza kimoyomoyo. "Sasa tutajificha wapi kwa muda huu wa kusubiri huu upepo mbaya upite?" Salha aliniuliza. "Kuna rafiki yangu mmoja.

Check image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 33

Nilimkatisha "Sasa wanawezaje kuwashawishi watu wote hao?" "Pesa inaongea. Ni kitu gani ambacho pesa inashindw" - 1997365338569021965
ReportShareDownload064

SALHA 33 Nilimkatisha "Sasa wanawezaje kuwashawishi watu wote hao?" "Pesa inaongea. Ni kitu gani ambacho pesa inashindwa kununua? Pesa inanunua haki, pesa inanunua ukweli. Kutokana na nguvu ya pesa hadi leo sijajua yupi ni mtu sahihi zaidi yako kumtwisha mambo haya katika kichwa chake" Nilikubali kwa kichwa. Saa moja ilikuwa imepita tangu tujadili mambo hayo na Salha. Hadi sasa tulikuwa hatujapata muafaka. Tuliwaza na kuwazua. Bado hatukupata njia sahihi ya kuwakabili wakina Nassoro. Bado tuliona hatari ilikuwa inatujia mbele yetu. Inatujia kwa kasi kubwa sana. "Sasa tunafanyaje ili kuepuka kisanga hiki Salha?. Maana tupo katika hali ya hatari sana. Kosa moja tu litasababisha vifo vyetu, lazima tutumie akili za ziada kuikwepa mikono haramu ya wale jamaa. Na lazima tufanye juu chini kumtafuta mtu ambaye tutamuelezea haya ili aweze kutusaidia.." Alinikatisha… "…nakubaliana na wewe Muu hundred percent, but the issue is... mtu huyo ni nani? Mtu tutakayeamini kwa asilimia zote kwamba yuko upande wetu" Aliniangalia usoni kwa macho yake laini yakiyomlenga machozi, akaendelea. "…na wale jamaa kwakuwa washajua kuwa niliyaona mambo yao waliyokuwa wanayafanya, lazima waongeze nguvu katika msako wao. Watusake, watukamate, watuue…" Salha aliongea huku machozi yakiwa yanamtiririka. "Usilie Salha. Amini hatutokufa, i will use my effort to ensure that jamaa tunawamaliza sisi, na mipango yao hasi tunaiweka hadharani. Amini tuko pamoja katika hali zote Salha. Nitakuwa na wewe bega kwa bega kuhakikisha haudhuriki, hauumii, hauteseki. Na nafanya haya yote kwakuwa nakupenda kwa moyo wangu wote Salha" Salha aliniangalia usoni. Alitabasamu huku akiwa analia. Alinikumbatia kwa nguvu. Mdomo wake ukiwa karibu na sikio langu la kulia. Alisema "…wewe ni mwanaume Muu, mwanaume shaba’bi. Mwanaume niliyekuwa namsaka usiku na mchana. Na leo nimempata. Ninajivunia sana kuwa na wewe Muu. Nakupenda sana. Nakupenda mno…" Alimaliza huku akinipiga busu la nguvu katika shavu langu. Busu lililonifanya nisahau hatari iliyokuwa inatukaribia kwa muda. Mara simu ya Salha iliita. Aliangalia simu yake. Namba ngeni" Alisema kwa sauti ndogo. "Pokea" Nilimwambia.