Check & Save & Download Instagram user photos and videos. List Most Popular Hashtags and Users. Recent Popular media and share themChecksta
  1. Homepage
  2. itaendelea

#itaendelea hashtag

Posts attached with hashtag: #itaendelea

lifestyles and history (@simulizi_tz) Instagram Profile Photosimulizi_tz

lifestyles and history

Check image by lifestyles and history (@simulizi_tz) with caption : "Part 6
Siku moja nilitoka nje usiku. Kwenye ile nyumba tulikuwa tunaishi na baba mwenye nyumba pamoja na mama yake mzazi" - 2007984079077566882
ReportShareDownload08

Part 6 Siku moja nilitoka nje usiku. Kwenye ile nyumba tulikuwa tunaishi na baba mwenye nyumba pamoja na mama yake mzazi. Nikiwa nimekaa pale nje nikaona kundi kubwa la watu wanapita yaani wanatoka upande wa chini kule ambako natazama wanaelekea juu ambako ni ndani ya jiko la mama yake baba mwenye nyumba. Nikabaki najiuliza ina mana hwajaniona pale nilipokuwa nimekaa? Lile kundi la watu liliingia kwenye nyumba ya msonge na wakajaa nankutosha mle ndani. Kalikuwa ni kajumba kadogo sana ambako kwa haki ya kawaida hata watu kumi hawatoshi kukaa nle ndani lakini lile kundi lote lilitosha mle ndani. Nilipoona vile nilisimama na kwenda kuchungulia kule walipokuwa. Macho yangu yalikutana moja kwa moja na macho ya yule bibi. Sikujua kama wale watu wengine waliniona au la. Nilipotoka pale nikarudi moja kwa moja kulala. Asubuhi yule bibi akaniita na kunielezea kila kitu. Alinambia yeye ni chanzo cha matatizo kwenye ile nyumba lakini mimi hajawahi kunigusa na chanzo cha matatizo yangu ni mama wa Mme wangu. Baada ya pale nikawa najiuliza ni kwa nini mama anifanyie hivi? Nilikuwa nimemkosea nini? Baada ya pale nikajiambia nitadili nae vizuri na kumbuka maneno yangu nikishajinenea huwa yanasababisha jambo kubwa au baya kwa Huyo anenewae. Jioni Mme wangu alinambia kuwa watu wanasachi nyumba ya mama yake na kusema kuwa yeye ni mchawi. Nilijikuta najiambia kuwa vita ndo imeanza. Sikutaka kumfanyia chochote yule mama kwani nilishajua kuwa yule ni bibi wa mwanangu. Nilipoona nimechoka sana nikaamua kurudi kwetu na baada ya pale Mme wangu alinifata, lakini kila siku roho yangu ikawa inaniambia nisubiri mtoto atembee ndio nipambane. Niliporudi kwa Mme wangu nilikuta mama mkwe kachukua kila kitu mle ndani yaani kasafisha kabisa. Nilirudi lakini mama mkwe akawa hanisumbui tena. Nilipofanya biashara zangu nikanunua kila kitu yaani vitu vipya na baada ya hapo mama mkwe akaanza tena. Mama mkwe wangu alikuwa na watoto watatu, wa kwanza wa kike, wa pili Mme wangu na wa tatu au wa mwisho alikuwa mdogo kabisa.... #Itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "DADA MANKA (07)

Tulianza kubadilishana mate palepale kwenye kabati, baada ya muda aliona anachelewa, mwanaume alinibeba" at Dar es Salaam, Tanzania - 2007597683486020407

DADA MANKA (07) Tulianza kubadilishana mate palepale kwenye kabati, baada ya muda aliona anachelewa, mwanaume alinibeba juujuu mpaka kitandani. Kwa vile mchicha ulikuwa umeishakolea nazi tuliumwaga juu ya ubwabwa na kuanza kujimegea tataribu. Mateja alionekana ana pupa kama mamba mwenye njaa, hakuchelewa kukifikisha chombo ukingoni mwa bahari. Baada ya mapumziko mafupi tulirudi ndani ya ngarawa kuendelea na safari, katika vitu ambavyo katika maisha yangu nilikuwa sivipendi ni usumbufu ndani safari. Ooh geuka hivi, lala hivi, inama hivi, nyanyuka hivi, kwa upande wangu niliona usumbufu lakini nilivumilia kwa vile ndiyo ilikuwa siku yetu ya kwanza kukutana. Kama ningekuwa nimemzoea ningempasha, kwani hakuna starehe ya mapenzi mpaka kusumbuana kumgeuza mwenzako kituko,ile kwangu sikuona mapenzi zaidi ya adhabu. Siku zote niliamini baada ya safari ndefu mtu humwaga mzigo na kutelemka. Siku ile tulikaa kaa mpaka saa tatu usiku baada ya kuoga na kula alinirudisha nyumbani. Kabla ya kuondoka Mateja aliniahidi vitu vingi ikiwemo kunijengea nyumba kuninunulia gari na kuyabadili maisha yangu kwa ujumla. Siku ile moja tu alinipatia laki tano taslimu, sikuamini niliona miujiza kupata raha na kiasi kikubwa cha pesa kama kile. Nilipofika nyumbani nilimkuta Bi Shuu yupo chumbani kwake, Nilifungua mlango wa chumba changu na kuingia ndani. Nilipowasha taa nilishtuka kumuona Bi Shuu kanisimamia nyuma, akuzungumza chochote ila alinikata jicho kali. “Shikamoo Bi Shuu” “Hainisaidii kitu” “Mbona hivyo mama yangu” “Kazi gani ya kutoka saa moja asubuhi kurudi saa tano za usiku?” Mmh, makubwa nimekuwa mtoto mdogo wa kuwa chini yake kwa kila kitu. Nilijua uchawi wa Bi Shuu ni nini, niliinama na kuchukua mkoba wangu na kufungua. Nilihesabu nyekundu tano na kumpa. “Za nini?” “Katumie tu” “Za kodi?” “Walaa, nimekutunuku tu mama yangu.” “Kweli!?” “Kweli unafikiri uliyonifunza madogo” Bi Shuu alifurahi na kunikumbatia na kusahau aliyobwatuka muda mfupi, baada ya kunipandisha na kunishusha alisema. “Weee mwana kulikoni” “Kaa chini nikupashe kazi imekuwa kaziiiii” “Usiniambie” “Habari ndiyo hiyo shilingi moja kwa sekunde ndio mpango” “Wacha wee leo Mchaga kawa mzaramu” #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Check image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "DADA MANKA (06)

Mateja alinipeleka kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano.
Kwa vile shida yake niliijua sikushtuka kum" - 2007573785138835246
ReportShareDownload036

DADA MANKA (06) Mateja alinipeleka kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano. Kwa vile shida yake niliijua sikushtuka kumsikia akiuliza chumba cha VIP, baada ya kulipia tulikwenda kwenye chumba kilichokuwa ghorofa la pili. Chumba kilichokuwa cha kifahari, ambacho kilikuwa kipo katika hadhi ya juu. Katika maisha yangu sikuwahi kuingia kwenye chumba kizuri kama kile. Chumba nilikiona kilikuwa kinapendeza lakini wasiwasi wangu bosi wangu atakipata alichokifikilia kukipata mwilini mwangu. Sikutaka nami kijiweka nyuma kwani nilikumbuka kauli za Bi Shuu mama mlezi wangu shangingi mstaafu, kuwa niwapo mbele ya mwanaume nijionesha nipo tayari kumpa kile anachokitaka. Siku zote aliniambia nijiamini ili kumfanya mwanaume naye ajiliuze mara mbili mbili ataniingiaje. Sikupoteza wakati baada ya kuingia tu chumbani nilivua nguo zote na kubakia kama kuku aliyenyonyolewa. Sikuchelewa kumsaula na yeye tukawa sale sale maua. Nilitembea kama miss kuelekea kwenye kabati kuchukua taulo kwa makusudi nimuoneshe umbile langu ambalo mwanzo huwa utata kwa wanaume. Lakini wakiisha nipata nakuwa kama Big G iliyotafunwa na kuisha utamu mwisho wake hutemwa. Kwa kweli sikupenda kutongozwa siku moja na siku hiyo hiyo kumvulia mwanaume nguo ya ndani. Niliamini kabisa kujilahisi vile lazima thamani yangu ingepungua lakini kama ningemzungusha, kidogo thamani yangu kwake ingepanda. Nilijua lazima ataniona maharage ya Msanga maji nusu kijiko. Lakini sikuwa na jinsi kutokana na njia aliyotumia kwa kweli nilijikuta siwezi kuuruka mtego wake mwepesi. Sikuwa ndege mjanja lakini nilinaswa kijinga sana, japo sikujua tatizo langu lakini nilipokuwa natembea na kumuachia umbile la nyuma lililokuwa linawatesa wanaume wengi. Niliinama makusudi kama najikuna mguu ili tu nizidi kumpagawisha. Kitu kilichofanya Mateja azidi kuwa katika wakati mgumu, wakati nafungua kabati nitoe taulo Mateja alikuwa tayari yupo nyuma yangu na kunikumbatia kwa nyuma. Nilijua uzalendo ulikuwa umemshinda, mambo yalianzia pale. Tulianza kubadilishana mate palepale kwenye kabati, baada ya muda aliona anachelewa, mwanaume alinibeba juujuu mpaka kitandani. #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Check image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "DADA MANKA 05 “Manka agiza chochote ukitakacho kwa bei yoyote.”
“Asante, nataka kula unachokipenda wewe,” utanishangaa k" - 2007571469908176683
ReportShareDownload042

DADA MANKA 05 “Manka agiza chochote ukitakacho kwa bei yoyote.” “Asante, nataka kula unachokipenda wewe,” utanishangaa kwa nini nimesema vile, nilifanya vile ili kumtoa wasiwasi na kumfanya awe huru kwangu japo si katika suala la mapenzi. “Hapana Manka nataka wewe leo ndio uchague chakula tutakacho kula.” “Sawa,” nilichagua chakula ambacho wote tulikuwa. Baada ya chakula wakati wa kunywa vinywaji Shaka aliniuliza. “Samahani.” “Bila samahani.” “Manka, umeolewa?” “Sijaolewa.” “Una mchumba sina?” “Sina.” “Rafiki wa kiume?” “Sina.” “Manka mbona unanidanganya.” “Kweli bosi.” “Hivi Manka kwa umbile alilokujali muumba usiwe na mwanaume?” “Si kwamba sijawahi mwanaume ila kwa sasa sina.” “Kweli?” “Kweli kwa nini nikufiche ili iwe nini?” “Mara nyingi watu wamekuwa si wakweli.” “Huo ndio ukweli wangu.” “Kwa nini mrembo kama wewe huna rafiki wa kiume?” “Sina bahati nimeamua kuishi peke yangu.” “Ina maana hata ombi langu litagonga ukuta?” “Ombi gani?” “Kwa vile huna mtu nilifikili unafaa kuwa mke wangu.” “Aaah, bosi,” kauli ile ilinishtua sikupenda kuisikia masikioni mwangu. Sikuwa na jibu la moja kwa moja, moyo mapigo ya moyo walinienda mbio na machozi yalinitoka. Mateja alishtuka kuniona nikitoka machozi badala kumpa jibu lake. “Manka vipi?” “Hataa,” nilitikisa kichwa. “Mbona machozi yanakutoka.” “Kauli yako imenishtua.” “Kivipi?” “Sikutegemea kuniambia neno hilo mapema kiasi hiki.” “Manka, penzi limuingiapo mtu huwa kama kichaa aliyekatikiwa na mishipa ya fahamu. Niyasemayo si mimi ni moyo wangu naomba unihurumie.” “Ni kweli, lakini sina bahati kila siku mapenzi limekuwa likinitesa.” “Kivipi?” “Mpaka leo sijajua sababu ya kuachwa na wanaume.” “Ni wazi wote waliopita walikuwa na tamaa ya kukujua ulivyo na si mapenzi ya dhati. Lakini nakuamini mimi ndiye mwanaume sahihi kwako.” “Hiyo kauli kwangu nimeizoea, lakini mwisho wa siku mambo huwa kinyume.” “Niamini Manka, nitakuwa mume mwema.” “Mmh nitashukuru, lakini usinitende utaniumiza.” “Siwezi.” Baada ya chakula tulirudi ofisini, hatukufanya sana kazi Mateja alikuwa na uchu wa fisi. Aliniomba tufunge ofisi twende tukastarehe, sikuwa na pingamizi nilifunga kazi na kuongozana naye kwenye gari lake. #ITAENDELEA

Vennita Mwita (@vennita_mwita) Instagram Profile Photovennita_mwita

Vennita Mwita

Check image by Vennita Mwita (@vennita_mwita) with caption : "#Kosa_langu #Hadithi_inaendelea 
#Sehemu_17 #Mtunzi @vennita_mwita ...Kondakta aliniruhusu nilale ndani ya basi baada ya" - 2006627419150205021
ReportShareDownload029

#Sehemu_17 #Mtunzi @vennita_mwita ...Kondakta aliniruhusu nilale ndani ya basi baada ya abiria woote kuondoka, na kwa kuwa basi lilikuwa halisafiri tena siku iliyofuata. Alinipatia na shilingi 5,000, ilikuwa pesa nyingi wakati huo. Nilimshukuru sana. Kwa uchovu, majonzi, huzuni nilijipumzisha katika siti ya nyuma ya gari, nikalala usingizi. Alfajiri niliamka, nikapanda daladala toka Ubungo hadi ilala,nikaenda katika kaburi la mama yangu, nikakaa juu, sehemu yangu ya faraja! nikamsimulia mama kila kitu. Sasa naelewa kwanini mama alisema sifa ya mtoto wa kiume ni ujasiri. Nakuahidi mama nitapambana! Jioni siki hiyo nilikwenda kumtembelea bibi Monica, kwani nilitaka niishi pale tena na nimlipe kodi mimi kwa vile sasa nilikuwa napata pesa kila siku kwa kubeba mizigo sokoni. Sikutaka sehemu nyingine maana nilihisi sitaweza kukaa sehemu mpya bila mama yangu, na pia wasingenipokea kama mtoto katika nyumba ya kupanga, walau bibi Monica ananifahamu, yamkini akakubali. Nilifika kwa bibi, nikamsalimia lakini alikuwa kalala akiwa hoi,nilijitambulisha, alinikumbuka, alilizwa na msiba wa mama yangu. Nilishangaa, kwani alikuwa mkali kwetu! Aliniambia alikuwa anaumwa sana ila alimuomba MUNGU, asife mpaka atakapo kutana nami, ili aniombe msamaha, na kuniachia nyumba yake kama urithi wangu ili niitunze! Sikuelewa! Aliniambia yeye hana watoto, hakuwahi kuzaa, ndio maana alikuwa na hasira nasi. Lakini sasa atakufa kwa amani kwani kanifanya mimi kuwa mjukuu wake, aliniomba nikamuite mjumbe na mwenyekiti wa mtaa, nilifanya hivyo. Bibi aliongea hayo maneno tena mbele yao. Mwenyekiti alimsainisha bibi na kunipa zile karatasi. Sikuamini, na sikujizuia kutokwa na machozi. Nilimkumbuka mama! Nilianza maisha mapya na bibi Monica. Nilimjali, nilichota maji, kusafisha nyumba yetu, kutafuta chakula na kuhakikisha bibi anakula na kunywa dawa pia. Baada ya miezi miwili bibi alifariki, sasa nilikuwa na akili, nilimutaarifu mjumbe, na mazishi yalifanyika. Bibi alizikwa jirani na kaburi la mama yangu. Kwa muda wa miezi hiyo miwili nilimuona bibi Monica kama ndugu yangu wa dhati, sikujihisi mpweke.. ? #Itaendelea..

Vennita Mwita (@vennita_mwita) Instagram Profile Photovennita_mwita

Vennita Mwita

Check image by Vennita Mwita (@vennita_mwita) with caption : "#Kosa_langu  #Hadithi_inaendelea 
#Sehemu_16 #Mtunzi @vennita_mwita ... Nafukuzwa na kutukanwa kama mbwa koko, mototo wa" - 2006055584847331230
ReportShareDownload276

#Sehemu_16 #Mtunzi @vennita_mwita ... Nafukuzwa na kutukanwa kama mbwa koko, mototo wa mdogo wako, nami nimetoka Dar kuja kukutafuta mjomba, kweli?" niliuliza haya maswali kwa sauti huku nikilia. ‘Ndio mimi, ni Mwalomgo; lakini sikufahamu, umefikaje hapa? Na hili kundi lote ni kina nani, na kwanini hamkufika mapema kama ni watu wazuri?’ Nilijieleza kwa kifupi, maana nilikuwa nalia sana. ‘Sasa ondoka kwa amani kwa kuwa ni usiku sasa, uje ofisini kwangu kesho asubuhi, tuongee, mimi ni Diwani, ofisi yangu iko hapo Karibu na standi, nitakusikiliza nijue jinsi ya kukusaidia zaidi, kwasasa umeisha muumiza mke wangu, na watoto wangu wanasoma kwa ajili ya mtihani kesho, hawahitaji kelele. Tayari hapa kuna hali isiyo ya Amani. kesho tutaongea zaidi mpwa wangu, usiku mwema, chukua hii elfu moja, utakunywa chai kabla ya kuja ofisini kesho. Niichukua ile pesa, kwa hasira nikaichana vipande vipande nikaitupa pale sebuleni, nikatoka njee. Wote walipigwa butwaa kwa muda! "Hata mimi najua kuitafuta, wape watoto wako, nitaishi na kaburi la mama yangu Dar mpaka siku nitakayo kufa." Ina maana mama yako kafarikiii? lini? Ebu nieleze vizuri, unaitwa nani?" inamaana unasema kweli kuwa wewe ni ndugu yangu sio kibaka?’ Aliuliza mjomba. "naitwa Paul, yatima. Kwaheri." Niliondoka na wale watoto, walisikitishwa sana kwa yaliyonipata, waliahidi kunisaidia. Haya ni baadhi tu ya mambo wanaotendewa watoto wengi majumbani baada ya kufiwa na wazazi wao. Niliamua kurudi Dar siku iliyofuata, ilinipasa kulivizia lile basi tena. Sikulia tena, kwani nilijipa moyo wa kupigana na maisha tu sasa. Watoto wenzangu walinichangia pesa walizokuwa nazo, walinisindikiza stendi kulisubiria basi. Tuliongea mengi, hatukulala tena usiku ule. waliahidi kuja Dar kutafuta maisha, niliwaelekeza nilipo, nami niliahidi kuwapokea na sote tungelala katika kaburi la mama yangu kwani nililizungushia miti na kuweka maboksi na nailoni juu, hivyo sikulowana kwa umande wa alfajiri. Nilimsimulia konda yaliyotokea. Alisikitika na kunipakia tena kurudi Dar, na kama kawaida,usiku sana tulifika Ubungo standi... #Itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "DADA MANKA (04)  Niliamini kabisa bosi kwa mtazamo wa nje alikuwa amepata bonge la mwanamke, lakini ndani sikuwa na sifa" at Dar es Salaam, Tanzania - 2006008034988693107

DADA MANKA (04) Niliamini kabisa bosi kwa mtazamo wa nje alikuwa amepata bonge la mwanamke, lakini ndani sikuwa na sifa zile za kukaa na mwanaume kwa muda mrefu. Niliyapuuza na kuendelea na kazi, nilikumbuka kuna kazi nilitaka kupata maelekezo kwa bosi. Nilimnyanyua simu kumpigia baada ya kuita kwa muda ilipokelewa. “Haloo bosi.” “Ooh..Aah…Nani Manka,” maskini bosi wangu alionesha kiwewe bado hakijamtoka. “Bosi mbona hivyo?” “Aah, kawaida tu, unasemaje?” “Ok, bosi nilikuwa nauliza hii kazi ya malipo kuna maandishi ya mkono nayo niyaandike?” “Hakuna tatizo, yaandike kama ilivyoandikwa.” Nilikata simu na kuendelea ka kazi yangu kama kawaida, baada ya muda nikiwa bize simu ya mezani iliita, nilinyanyua na kupokea. “Haloo bosi.” “Ndiyo Manka jiandae tukapate lunch.” “Nashukuru bosi.” Baada ya kukata simu, niliangalia saa kubwa ya ukutani iliyokuwa mbele yangu, ilionesha ni saa saba kasoro kumi mchana. Nilimalizia kazi yangu ili nipate muda wa kwenda kula, nikiwa bado nimeinama nikirekebisha tatizo la kisarufi nilishtuliwa na sauti ya bosi. “Manka tunaweza kwenda.” “Hakuna tatizo bosi, namalizia kurekebisha sarufi.” “Utamalizia tukirudi.” Nilisave kisha nilizima computer na kunyanyuka, nilijitengeneza vizuri nguo niliyovaa. Kwa chati nilimuona bosi wangu koo likimcheza kama mtu mwenye kiu kikali. Baada ya kuhakikisha nipo sawa tulitoka hadi kwenye gari lake kisha tulikwenda kwenye moja ya hoteli ya kifahari ambayo ilinikumbusha mbali enzi nipo kwenye ndoa yangu. Tulipofika Mateja alionesha kutojiamini sana kwangu kitu ambacho sikuamini mwanaume kama yeye kuwa katika hali ile. Sikuwa na sifa kubwa zaidi ya mwanamke aliyepoteza matumaini ya kupata hadhi mbele ya mwanaume. Niliamini kaniona kwa nje hanijui ndani nilivyo ndio maana ananipapatikia. Nilijua akikipata anachokitafuta kwangu pengine ndiyo siku ya kunifukuza kazi, lakini sikuwa na jinsi kila mwanaume mwenye pesa aliamini mwanamke sahihi wa kukaa naye ni mimi. Baada ya kuketi kwenye viti vyetu muhudumu alifika na kutaka oda zetu. “Manka agiza chochote ukitakacho kwa bei yoyote.” “Asante, nataka kula unachokipenda wewe,” utanishangaa kwa nini nimesema vile, #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "DADA MANKA (02)  Baada ya kufika nilikaa mwa muda wa mwezi mmoja na kunitafutia kibarua katika kiwanda kimoja, ajabu msi" at Dar es Salaam, Tanzania - 2005710283159684000

DADA MANKA (02) Baada ya kufika nilikaa mwa muda wa mwezi mmoja na kunitafutia kibarua katika kiwanda kimoja, ajabu msimamizi alinizimikia na kuanzisha mahusiano na mimi. Kwa vile kila mmoja alikuwa na ujiko kuwa na uhusiano na bosi basin a mimi nilimkubalia. Kama kawaida haikuchukua hata mwezi akanimwaga na kashfa nyingi kwamba heri atembee na mwanaume mwenzake kuliko kulala na mimi. Kwa kweli kitendo kile kilizidi kunidhalilisha na kuniweka kwenye wakati mgumu, kibaya kila mwanaume niliyekuwa nakutana naye na kuniacha hakunieleza tatizo langu. Kwa kweli niliumia sana na kuamua kuacha kazi, niliapa sitakuwa tayari kufanya kazi wala kuanzisha uhusiano na mwanaume yeyote. Baada ya shoga yangu kupata bwana ilinibidi nihame kwa kutafutiwa chumba sehemu za uswahili kwa bibi mmoja maarufu pale mtaani Bi Shuu, ni bibi wa miaka 55 lakini mambo yake temea chini. Bibi yule alinilea kama mwanaye wa kuzaa hata kodi yangu hakuitaka. Kuhamia kwa Bi Shuu nilijikuta nikiingia dunia nyingine kabisa, kweli nimekubali tembea uone mambo, ningekaa Arusha ningeyajua haya. Nazidi kukubali kweli vikiungwa vitamu, tena mtu ataomba aongezwe na akimaliza kula lazima ajilambe vidole. Najua una hamu kuvijua hivyo vitamu vilivyo ungwa mpaka watu wakajilamba, Naomba twende pamoja tuipate wote faida ya kuwa karibu na makungwi kama Bi Shuu. ******** Katika mambo niliyokuwa siyapendi katika maisha yangu ni pamoja na kusumbuliwa na mwanaume wakati wa kilimo cha mhogo. Ooh! Inama, mara jipinde hivi, mara geuka hivi. Siku zote nilijiuliza kwani bila kukusumbua hivyo mwanaume hawezi kufikisha mzigo wake. Kitendo cha kijana huyu ambaye alinipata kupitia kwa Bi Shuu kutaka kunisumbua kilinikera sana. “Manka mbona hivyo sasa raha ya mapenzi ipo wapi?” “Nimesema sifanyi unavyotaka, sipo kwenye mazoezi ya yoga hapa kama huwezi hivi, vaa nguo zako ondoka, ” nilisema kwa ukali bila kumuangalia nyuma yangu alipokuwa amekaa. “Lakini Man…,” “Ee..ee..eeh, nasema hivi kwani tatizo nini bila hivyo unavyotaka hufiki safari yako?” Nilimkata kauli Edward. “ Edward alikosa la kujibu na kuamua kufanya mpaka alipomwaga na kuvaa nguo zake na kuondoka na tokea siku hiyo hata Salam alikuwa hataki kunipa. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MUME WANGU -03

Siku mbili baada ya kuanza zamu ya usiku kazini, nilihisi kukosa utulivu na nilikuwa nikimpigia simu mum" at Dar es Salaam, Tanzania - 2004265369809021168

MUME WANGU -03 Siku mbili baada ya kuanza zamu ya usiku kazini, nilihisi kukosa utulivu na nilikuwa nikimpigia simu mume wangu mara kwa mara na kumuuliza kama yuko salama. Mume wangu aliniambia kuwa kila kitu kipo shwari na yeye yuko salama, hivyo sikuwa na wasiwasi kuhusu chochote. Saa moja baadaye usiku wa manane, nilipata ujumbe wa simu kutoka kwa mume wangu akiniambia: “Belinda alikuja chumbani kwetu akiwa mtupu na kutaka nifanye nae mapenzi”. Nilihisi kama nataka kuanguka, nikawa na maswali mengi kichwani, itakuwaje kama kweli alifanya, na sasa anataka kujisafisha na kujionesha kuwa ni mwanaume mwema? Ni wanaume wachache sana wanaoweza kukataa ofa yenye majaribu kutoka kwa msichana mzuri na mrembo. Baada tu ya kumaliza kusoma ujumbe wa mume wangu, nilipokea ujumbe mwingine kutoka kwa Belinda akisema kuwa kuna kitu muhimu anataka kuniambia. Usiku ule ulikuwa mrefu kwangu, sikuweza kuweka nguvu kwenye mambo mengine. Ilipofika saa 10 alfajiri, niliomba ruhusa na nilidanganya kuwa mwanangu anaumwa, hivyo nilihitaji kuondoka mapema. Nilipewa ruhusa nilipofika nyumbani Belinda alianza kulia akisema kuwa hajui kilichomtokea na kwamba ana hofu sana. Aliponieleza, ndipo nilipoamini kuwa mume wangu alikuwa akisema ukweli. Nilipoingia chumbani kwetu mume wangu alinyanyua na tukakumbatiana kwa dakika kadhaa. Nilijivunia sana kuwa nae na kuona kuwa mimi ni mwanamke mwenye bahati, ilikuwa ajabu sana. Nilichanganyikiwa mno kwa sababu Belinda ni mpwa wangu ambaye nilimpenda sana. Ni binti wa marehemu kaka yangu na niliahidi kumlea mpaka atakapoweza kujitegemea, sasa nilifanya kosa gani kumchukua? Nikimfukuza nyumbani, ataenda wapi? Sijui mama yake mzazi alipo, nitafanyaje sasa? #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MUME WANGU-02

Mwaka mmoja na nusu tulikuwa katika maelewano mazuri, lakini baada ya kujifungua mtoto wa 3, Belinda alia" at Dar es Salaam, Tanzania - 2003814613435831199

MUME WANGU-02 Mwaka mmoja na nusu tulikuwa katika maelewano mazuri, lakini baada ya kujifungua mtoto wa 3, Belinda alianza kubadilika. Ushauri wangu kwake haukuwa na maana yoyote, alimsikiliza Moses tu. Alikuwa akinitazama na kusema kuwa mimi ni mnene sana na kwamba wanaume wanapenda wanawake wembamba kama yeye. Mwanzoni ilionekana kama utani tu lakini baadaye ikawa kama mazoea. Nilikuwa nikimwambia kuwa wanaume wanatofautiana katika uchaguzi wao na pia mimi sikuwa mnene sana kama alivyokuwa akiongeza chumvi. Siku moja tulikuwa tukitazama mashindano fulani kwenye televisheni, akaanza kucheka kwa sauti kubwa huku akinyoosha kidole kwa mmoja wa washiriki wa mashindano na kusema: “Shangazi Faith, usipoangalia uzito wako utaishia kuwa kama yule”. Mwanamke aliyemuelezea alikuwa na kilo 442, nami nilikuwa na kilo 60. Hapo mume wangu akaonekana kusononeka na kumwambia kuwa nilikuwa na uzito sahihi na mzuri hata kama nina watoto 3 na akamuonya asirudie kuzungumza nami kwa namna ile… Ukweli mimi sikuchukulia kuwa ni tusi kwa sababu alikuwa mtu wa karibu mno kwangu, lakini mume wangu aliposema vile, akawa kama amenifungua macho. Siku zilivyozidi kusonga mbele, nilibaini kuwa Belinda ni binti mtata na ni kumridhisha. Alitaka vitu vingi, sikushangaa kwamba ilikuwa vigumu kwake kuishi na mama yake wa kambo, ambaye alikuwa mwanamke mzuri na mwema. Jioni moja ya Jumapili kabla sijaanza zamu ya usiku kazini kwangu, alianza kuniambia kuwa mimi ni mwanamke mzuri na kwamba nina bahati sana kuolewa na mwanaume kama Moses. Alinieleza waziwazi kwamba angependa kupata mume kama yeye. Jioni ile nilishawishika kuamini kwamba alikuwa akimtaka mume wangu lakini nilimwambia kuwa anatakiwa kuweka macho yake kwenye masomo, Mungu atampa anayoyatamani! Nilishindwa kukaa nalo, nilimpigia simu Hamasa na kumwambia kuhusu jambo hilo. Alinishauri niwe makini sana na Belinda. Siku mbili baada ya kuanza zamu ya usiku kazini, nilihisi kukosa utulivu na nilikuwa nikimpigia simu mume wangu mara kwa mara na kumuuliza kama yuko salama. #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Check Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MUME WANGU 01

Baba yangu alifariki dunia nilipokuwa darasa la 3. Ni siku ambayo ilibadilisha maisha yetu kutoka kwenye " at Dar es Salaam, Tanzania - 2003810700267717547

MUME WANGU 01 Baba yangu alifariki dunia nilipokuwa darasa la 3. Ni siku ambayo ilibadilisha maisha yetu kutoka kwenye hali nzuri kwenda kwenye hali mbaya. Mama yangu alikuwa mama wa nyumbani na alitegemea moja kwa moja kipato cha baba yetu. Kuanzia hapo, mama yangu akachukua jukumu la matunzo yangu na kaka yangu mkubwa George. Ndugu wa baba yangu walichukua mali zetu zote ikiwemo nyumba tuliyokuwa tukiishi. Baada ya miaka miwili ya tabu na mateso, hatimaye mama yangu alipata kazi kama mfanya usafi kwenye eneo ambalo baba yangu alikuwa akifanya kazi. Nilipofika darasa la 7 na kaka yangu akawa amefika chuo, mama yetu kipenzi alifariki dunia. Hakuna aliyekuwa tayari kutuchukua mimi na mtoto wa kaka yangu, Belinda aliyekuwa na umri wa miaka 4. George alipata mtoto nje ya ndoa alipokuwa kidato cha 3, mwaka mmoja baada ya kifo cha baba yangu. Mama ndiye aliyekuwa akimhudumia mtoto huyo tangu alipozaliwa. Mungu ni mkubwa, rafiki mkubwa wa mama yangu kutoka kanisani, Jessica alituchukua. Alikuwa mjane mwenye mtoto mmoja tu. Binti yake, Hamasa na mimi tulikuwa kama mtu na dada yake, hivyo tulipendana sana. Shangazi Jessica alikuwa mtu mzuri na mwema, alituhudumia kama watoto zake halisi. Kaka yangu alikuwa akija siku za likizo mpaka alipohitimu masomo yake. Nilichagua kusomea uuguzi baada ya kuhitimu masomo yangu ya kidato cha sita kwa sababu nilitaka kuchukua kozi ambayo itakuwa rahisi kupata kazi. Nikiwa mwaka wa mwisho chuoni, nilikutana na mume wangu Moses na tulifunga ndoa baada ya mwaka mmoja na nusu wa mahusiano yetu… Baada ya kujifungua mtoto wangu wa pili, kaka yangu George alifariki dunia katika ajali ya gari. Hakika nilichanganyikiwa sana. Mimi na kaka yangu tulipendana sana na tulielewana mno. Aliacha mke na watoto wanne. Belinda hakuweza kuwa na maelewano mazuri na mama yake wa kambo, hivyo nilimchukua. Sikutaka apate usumbufu kwenye masomo yake. Wakati huo alikuwa kidato cha 3 na niliamini kuwa atafaulu vizuri sana. Mwaka mmoja na nusu tulikuwa katika maelewano mazuri, lakini baada ya kujifungua mtoto wa 3, Belinda alianza kubadilika. #ITAENDELEA